• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe |
Buchosa District Council
Buchosa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Misitu
    • Biashara
    • Ushirika
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Telesenta
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi idhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Katibu Mkuu CCM Taifa aagiza Uharikishaji wa ujenzi wa barabara ya Nyehunge Sengerema Kukamilika kwa wakati Wilayani Buchosa

Posted on: August 14th, 2024

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa aagiza uharakishaji wa Ujenzi wa barabara ya Sengerema Nyehunge nyenye urefu wa kilomita 54.3 kwa kiwango cha lami kukamilika kwa wakati Wilayani Buchosa Mkoani Mwanza.

Agizo hilo amelitoa leo 14/08/2024 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emannue John Nchimbi wakati akiongea na wananchi wa Buchosa akitokea mkoani Geita ambapo amesema Viongozi na watendaji wanatakiwa kusimamia kikamilifu mchakato wa kupata wakandarasi  wenye uwezo na sikuweka watu kwa majaribio.

“Ni muhimu sana kujiridhisha kuhusu uwezo wa wakandarasi kabla ya kupewa kazi na kufahamu  historia zao za nyuma,kuna wengine tayari wanarekodi za  kuharibu kila sehemu duniani waliko kwenda na kukimbilia kwetu kama sehemu ya kujifichia na kuja kutuharibia kazi”.Amesema Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi.

Aidha Balozi Nchimbi wameshukuru wananchi kwa heshima kubwa na mapokezi waliyo yaonyesha wakati wa zira yake, ambapo amesema kwamba Serikali itaendelea kuwathamini kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Erick Shigongo ameshukuru na kutoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha nyingi zaidi ya shilingi Bilioni 63 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu,Afya,Maji na Miundombinu ambapo Serikali imeweza kujenga chuo cha Ufundi kilichopo Kata ya Nyehunge kijiji  cha Kayenze kwa fedha kutoka Serikali kuu, vyumba vya madarasa,Vituo vya Afya pamoja na Zahati.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Buchosa amesema jukumu lake ni kutekeleza ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ambayo alikabidhiwa ili asimamie ikiwa pamoja kuwaletea maendeleo wananchi “Kazi na inafanyika, CCM inafanya kazi kubwa,Buchosa iko salama kura ziko salama” Amesisitiza Mhe,Erick Shigongo mbunge wa Jimbo la Buchosa.

Mbunge wa Jimbo la Bochosa Mhe.Erick Shigongo akiongea na wananchi wa Buchosa leo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi,ambapo amesema wananchi waendelee kumwanini na yuko tayari kuleta maendeleo katika Jimbo la Buchosa.

Mamia ya wananchi wa Buchosa wamejitokeza kwa wingi leo  katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akitokea Mkoani Geita ambapo aliongea na wananchi na Kuahidi ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Sengerema kwenda Nyehunge yenye zaidi ya urefu wa kilomita 54.

 

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA UMMA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 26, 2024
  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA USAILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGAKURA(BVR)-2024 August 02, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA July 17, 2024
  • TANGAZO LESENI ZA BIASHARA 2024 July 10, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Halmashauri ya Buchosa yapongezwa kwa kupata Hati safi

    April 28, 2025
  • Halmashauri ya Buchosa yapongezwa kupata Hati safi

    April 28, 2025
  • DC Ngaga asisitiza Mahusiano mazuri kazini Buchosa

    April 03, 2025
  • DED Benson Mihayo awataka watumishi kushirikana katika ukusanyaji Buchosa

    March 27, 2025
  • Angalia zote

Video

UTOAJI WA MIKOPO HALMASHAURI YA WILAYA YA BUCHOSA
Video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Mpango Mkakati Wa Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Mkoa wa Mwanza
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
  • Wizara ya Kilimo

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

freevisitorcounters's Website

Location Map

Wasiliana nasi

    Buchosa District Council

    Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA

    Simu: 0759941297

    Simu ya kiganjani: 0765029662

    Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa