UMILIKI WA ARDHI
Utaratibu wa utoaji wa miliki – Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
1.Mahitaji ya umilikishaji wa miliki mhusika/mwombaji miliki anatakiwa awe na vitu vifuatavyo:
• Ramani ya eneo husika.
• Uraia.
• Mkataba wa mauziano/uthibitisho toka kwa mwenyekiti wa Serikali ya kijiji/kitongoji kama alimilikishwa kienyeji.
• Aandike barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ikipitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata kilipo kiwanja hicho na kwa mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho.
• Muombaji/mhusika atajaza mbalimbali atakazo pewa.
2.UMILIKISHWAJI
(A) Umilikishwaji wa “Allocation Letter” (miliki).
Utaratibu wa kuandaliwa “Allocation Letter unafuata baada ya mhitaji kukamilisha mahitaji yote ya umilikishwaji. Utaratibu huo ni:-
• Kufungulishwa file la kiwanja hicho.
• Matumizi ya kiwanja hicho kutolewa na Afisa Mipango Miji.
• Makadirio ya kodi ya ardhi kuandaliwa na mthamini.
• Maandalizi ya “Allocation Letter” yanakamilishwa.
(B) Utoaji wa Hati miliki
Utoaji wa Hati hufanyika baada ya kuandaliwa “Allocation Letter”. Iwapo hakutakuwa na allocation letter hati haiwezi kuandaliwa. Utaratibu wa kuandaa hati ni kama ifuatavyo:-
• Ushuhuda wa malipo ambayo huandaliwa baada ya mhitaji/mmiliki kulipia ada za Serikali zilizoainishwa kwenye “Allocation Letter”.
• Maombi ya ramani na maandalizi ya ramani hufanyika (Request for Deed Plan).
• Mpima huandaa Ramani za Hati na kuzipitisha .
• Maandalizi ya Hati miliki yanafanyika.
• Mhusika anasaini Hati miliki kwa kushuhudiwa na wakili au Mwanasheria.
• Maafisa Ardhi Huandaa Historia ya kiwanja hicho, na kupeleka kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya saini na usajili.
• Mhusika hufuata Hati yake kwa msajili wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
LESENI ZA MAKAZI
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa